Karibuni wote kwenye tovuti ya Kanisa la Biblia Publishers
Kanisa la Biblia Publishers ni idara ya Maandiko ya Kanisa la Biblia Tanzania. Kazi yake ni kutafsiri, kuandaa na kutoa maelezo ya Biblia kwa kiswahili. Tunachapisha vitabu kwa msomaji wa Biblia anayetaka kuelewa vizuri zaidi, ili apate kuelewa mwenyewe, kuwafundisha wengine neno la Mungu na kutafsiri maana yake kwa maisha ya kila siku. Kanisa la Biblia Publishers inadhamiria kukuza ufahamu wa Biblia Afrika Mashariki kwa njia ya kusambaza maandiko ya Kikristo yanayosaidia kuelewa Maandiko kwa manufaa binafsi, kwa kukua kiroho na kwa kutoa mafundisho.

Hongera kwa nia yako ya kusoma Neno la Mungu. Tunategemea tunaweza kukusaidia kwa njia mbalimbali kuelewa na kutangaza Neno la Bwana na kuhubiri ujumbe wa Bwana Yesu kwa watu walio karibu na walio mbali. Chunguza tovuti hii vizuri ili ujipatie vitabu vinavyofaa kwa maisha na huduma yako. Vitabu vyetu vinapatikana katika maduka mbalimbali ya Kikristo katika nchi ya Tanzania.

Mkuu wa Kanisa la Biblia Publishers
Dodoma, TanzaniaVitabu vipya vilivyotolewa karibuni

Masomo Bunifu ya Biblia

Masomo Bunifu ya Biblia

Muhtasari mpya ya milenia mpya kwa ajili ya kuwafundisha watoto wenye umri wa miaka 4 12 Neno la Mungu kwenye mfululizo wa muda wa miaka nane. Wahi! Ujipatie kwa ajili ya darasa lako la watoto! ...

[ Soma zaidi ]
Msamaha wa dhambi

Msamaha Wa Dhambi Na Hakikisho La Amani Na Mungu

Kile ninacho nuia katika kijitabu hiki ni kwamba kwa baraka za Mungu, uweze kumpokea Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi wako; na ikiwa umeshampokea uweze kujua kwa uhakika kwamba una uzima wa milele. ...

Bonyeza hapa kupakua kitabu hiki:
[ Pakua PDF ]
Wito wa Viongozi wa Kikristo

Wito wa Viongozi wa Kikristo

Waraka wa kwanza kwa Wakorintho sura nne za kwanza zina ujumbe unaohusu sana viongozi wa Kikristo katika ulimwengu wa leo. Kuna ujumbe wa pekee kwa ajili ya viongozi wa kanisa la leo, wawe ni wasimikwa au ni walei, wenye huduma ulimwenguni au kanisani ...

[ Soma zaidi ]

Emmaus Shule ya Biblia kwa Njia ya Posta

Emmaus ECSEmmaus Shule ya Biblia kwa Njia ya Posta inahudumia watu wote wanaopenda kusoma Biblia kwa njia ya posta. Masomo na mitihani yanatumwa kwa mwanafunzi. Baada ya kujaza anarudisha mtihani kwenye ofisi zetu. ...

[ Soma zaidi ]
 

Wasiliana nasi

Kanisa la Biblia Publishers
P.O.Box 1424, Dodoma
Tanzania

Phone: +255 (0) 26 2354 500
Mobile: +255 (0) 713 609166
Email: contact@klb-publishers.org

Location: Dodoma, Ipagala,
Eneo la Emmaus, off Dar Road

Washiriki wetu